MAREKANI YAIPA ONYO MSUMBIJI

 Marekani imetahadharisha kuwa makundi ya wanamgambo yameendelea na operesheni zake nchini Msumbiji katika eneo la Kaskazini la Cabo Delgado huku yakiungwa mkono na wanamgambo wa Islamic State.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia vijiji mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.


Mkuu wa operesheni maalum ya Marekani barani Afrika Meja Jenerali Dagvin Anderson, amewaambia wanahabari kuwa kundi hilo limekuwa likipata msaada kutoka nje, hali inayolifanya kundi hilo kuwa hatari zaidi.


''Tumewashuhudia katika kipindi cha miezi 12 mpaka 18 wakiimarisha uwezo wao wao, wa mashambulizi, na kutumia mbinu ambazo hutumika pia katika maeneo mengine ya ulimwengu- Mashariki ya Kati ambako kuna makundi yenye uhusiano na Islamic State'', alisema Jenerali Anderson


Uasi wa wanamgambo wa kiislamu waliojitokeza katika kona ya mbali ya Msumbiji umegeuka kuwa vita vya wazi katika wiki za hivi karibuni, na ripoti za mauaji ya watu, kukatwa kichwa na kutekwa nyara kwa miji miwili katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado, aliandika mwandishi wa BBC Africa Andrew Harding mwezi Mei


Watu wenye silaha walitembea taratibu katikati ya majani marefu, wakipita kando ya jengo kubwa jeupe wakionekana kutosumbuka kabisa na mlio wa risasi.


Wengi wakiwa na silaha na walivaa aina mbalimbali za mavazi yaliyoonekana kuwa ya jeshi la Msumbiji. Milio michache zaidi ya risasi ilisikika kwa mbali na mmoja alipaza sauti ''Allahu Akbar''- Mungu ni Mkubwa.


Picha ya video, iliyopigwa mwezi Aprili kwa simu ya mkononi wilaya ya Muidumbe ulikuwa ushahidi wenye nguvu kuwa mzozo uliokuwa gizani katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji sasa umekuwa katika eneo la wazi kabisa kwa namna ambayo ni ya hatari.


Video ya pili, iliyochukuliwa majuma machache kabla, ilimuonesha mtu mmoja aliyekuwa amekufa, askari akiwa amelala kwenye dimbwi la damu. Kamera kisha zikatembea na kunasa mwili mwingine, kisha mwili mwingine ukiwa chini ya gari nyeusi ya polisi, kisha ikarekodi mwili wa nne ukiwa sehemu ya wazi, na kisha rundo kubwa la silaha kwenye eneo ambalo linaonekana kuwa ghala la silaha la polisi au jeshi.



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form