WALINZI WA MAKAMU WA RAIS WASHAMBULIWA KWA RISASI

 Walinzi sita wa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, James Wani Igga wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya msafara wao wa magari kuvamiwa na waasi mjini Juba. Kiongozi huyo hakuwa katika msafara huo wakati shambulio hilo lilipotokea. 

Msemaji wa Kiongozi huyo, Kalisto Lado amesema magari ya msafara yalichomwa moto na kikundi cha kijeshi cha National Salvation Front (NAS) ambacho kilikataa kusaini mkataba wa amani 2018

Makamu wa Rais hakuwepo katika msafara huo wakati shambulio. Aidha Msemaji wa Makau wa Rais amesema ni kikundi hiko pia kilimua mpita njia

Sudan Kusini imekuwa na machafuko tangu mwaka 2013 na hivi karibuni wasemaji wa Benki Kuu walihusisha machafuko kuathiri uchumi wa nchi hiyo na kushusha thamani ya fedha yao.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form