Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ameshutumu vikali kitendo kilichofanywa na vijana wahuni wanaodaiwa kukodiwa na kuushambulia kwa mawe msafara wa mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mkuu wa KKKT dayosisi ya Kaskazini Askofu Shoo aliyetaka serikali ya mkoa kudhibiti vitendo hivyo ili kulinda Amani ya nchi.
Akinukuliwa na gazeti la Nipashe la leo Anna Mghwira alisema vitendo vilivyofanywa si vya kistaarabu na atachukua hatua na kutoa taarifa siku chache zijazo.
Wananchi wamekuwa wakimtuhumu Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya kufadhili vikundi hivyo vya wahuni kushambulia mikutano ya Chadema kutokana na kujiapiza hadharani kwamba atatumia mamlaka yake kuhakikisha Freeman Mbowe hatashinda Tena ubunge katika Jimbo Hilo.