NEC KUKAGUA MAJINA YA WADHAMINI WA WAGOMBEA

 Afisa wa Tume anayehusika na habari na Mawasiliano, punde ametoa ufafanuzi kumtu Kupitia TBC1 kuhusu wagombea waliowaiting room kuwa, kuchelewa kwa baadhi ya wagombea kuingia chumba maalum cha uteuzi/kupokelewa fomu zao kunatokana na zoezi la uhakiki wa fomu zenyewe na uhakiki wa wadhamini. Tume ni lazima ijiridhishe kama waliomdhamini mgombea ni kweli kuwa ni wapiga kura. Na mambo mengine

Kwa wale waliopeleka kabla majina hayo kukaguliwa ktk ngazi ya Jimbo au kupelekea tume kabla, zoezi hili kwao ni la haraka zaidi, ila kama hukuwa umepeleka majina hayo kabla, basi itabidi uwe mpole kidogo kujiridhisha.

Pia ameeleza kuwa, wagombea wote ambao wamefika kituoni hapo kabla ya saa 10 watasikilizwa hadi waishe, isipokuwa kama mtu atafika baada ya saa 10. Kwa hiyo wale walio na wasiwasi kuhusu wagombea wa vyama vyao hasa CHADEMA, bila shaka wote watapata hiyo fursa ya kusikilizwa na Kkwasilosha fomu zao za uteuzi na baadae kuteuliwa kama wamekidhi vigezo vyote kwa kadri ya taratibu walizopewa. Wandugu tuwe na subira.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form