JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es salaam leo Tarehe 21.08.2020 amehitimisha ukaguzi rasmi katika wilaya ya Mwabepande Kinondoni. Ukaguzi huo ulifanyika katika mikoa mitatu ya Temeke, Ilala na Kinondoni kwa wilaya 13 za kipolisi za jiji la Dar es salaam.
Ukaguzi huu uliangazia utekelezwaji wa amri mbalimbali na usimamizi wa sheria za nchi ili kuona kama vinatekeklezwa kwa mujimbu wa viwango vinavyotakiwa na vinavyokidhi matarajio ya wananchi.
Aidha ameridhishwa na utayari wa askari, utayari ambao unawezesha askari kukabiliana na yeyote ambaye ataleta uvunjifu wa amani katika kipindi cha kampeni, kupiga kura, kutangazwa matokeo na kushangilia ushindi.
Pia Kamanda amewataka wanasiasa kwa kipindi hiki kuelekea katika kampeni za Urais, Ubunge na Udiwani wanatakiwa kutii sheria za nchi na wajiepushe na vurugu, lugha matusi ili kuhakikisha kwamba usalama wa nchi hauguswi kwa kwa namna yoyote ila kwa sababu ya kampeni.
SACP- LAZARO B. MAMBOSASA,
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
21/08/2020.