MCHUNGAJI ELIONA KIMARO WA KKKT APEWA LIKIZO YA SIKU 60

 

 
Kufuatia semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo na rasmi jana ameaga usharika wa KKKT Kijitonyama.
Mchungaji Kimaro amesema anatumia fursa hiyo kuwaaga usharika wa KKKT Kijitonyama na kuanzia kesho (yaani leo) Mchungaji Anna ataendelea kuwa Mchungaji wa Kanisa hilo, alisema Mchungaji Eliona Kimaro.
 
 
Kwa mujibu wa barua hiyo ilisema Mchungaji Kimaro atarudi tarehe 17/03/2023 na barua inamuelekeza kuripoti makao makuu na sio usharika wa KKKT KIJITONYAMA ambapo atapangiwa sehemu nyingine.
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninaye heshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyo elekezwa asante" alisema

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form