HIZI HAPA NAULI MPYA ZA MABASI YAENDAYO KASI (DART)


Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umetoa bei mpya za nauli kwa watu wazima wanaosafiri katika njia kuu na mlishi zitakazoanza kutumika leo ambazo zimeidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafi ri Ardhini (LATRA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa Dart, William Gatambi, viwango vya bei zilizotolewa kwa watu wazima vinaonesha kuwa watumiaji wa njia kuu kutoka Kimara kwenda kivukoni, Morocco na Gerezani ni Sh 750 na wanafunzi Sh 200 na kutoka Ubungo kwenda Kivukoni na Gerezani Sh750 na kutoka Morocco kwenda Kivukoni na Gerezani Sh750 na kwa wanafunzi ni Sh 200.
Wakati hapo awali viwango vya nauli kwa njia kuu kutoka Kimara kwenda Kivukoni, Morocco na Gerezani ilikuwa Sh 650 kwa watu wazima na kwa wanafunzi ilikuwa Sh 200 na kutoka Ubungo kwenda Kivukoni na Gerezani ilikuwa 650, wanafunzi ilikuwa Sh 200.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form