WASAFI TOWER YAKAMILIKA

 imeelezwa kuwa Wasafi Tower imekamilika kwa kiasi kikubwa na siku sio nyingi huwenda ukufanyika uzinduzi wake.

Mei mwaka huu Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa ujenzi au ujio wa jengo jipya la Wasafi Tower umekamilika kwa asilimia 80.

Akizungumza hii leo kwenye kipindi cha Goodmoring, Mtangazaji wa Wasafi Media, Mauldi Kitenge amesema kwa sasa kilichobaki ni vitu vichache sana vya kumalizia.

Ikumbukwe Diamond ambaye anamiliki lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB), pia ni Mmiliki wa Wasafi Media, Zoom Xtra (kampuni ya kutengeneza video), huku akiwa amefanya miradi mikubwa yenye mafanikio kama Diamond Karanga na Chibu Perfume.



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form