WAUAJI WAACHIWA HURU

 MAHAKAMA Kuu Kanda ya Kigoma, imewaachia huru washtakiwa 11 waliokuwa wakikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia askari wawili wa Jeshi la Polisi na kukata sehemu za siri za mmoja wa askari hao katika mapigano yaliyotokea wakati wa kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Hifadhi ya Ranchi za Taifa (NARCO), wilayani Uvinza.

Hukumu hiyo ilisomwa Ijumaa (Agosti 14), na kesi hiyo ilihusu tukio lililotokea Oktoba, mwaka 2018, wakati wananchi karibu 1,000 walipojiunga kupambana na askari wakiwa na silaha za jadi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Ilvi Mgeta, alisema sababu za kuwaachia huru ni ushahidi alioutoa daktari wa Kituo cha Afya cha Lugufu, aliye wahudumia baadhi ya washtakiwa na kueleza kuwa risasi walizopigwa zilipita juu ya ngozi wakati washtakiwa wana makovu makubwa yanayoonyesha risasi zilipita upande mmoja na kutokea mwingine tofauti na shahidi ulivyoeleza.

“Tunashindwa kuelewa kwa nini shahidi huyu alitoa ushahidi wenye nia ya kuidanganya mahakama wakati akiwa anajua ukweli ni ushahidi wa askari walioeleza kuwapo katika mapigano hayo.”

Ushahidi mwingine ulioelezwa kuwa dhaifu ni wa askari walioeleza kushiriki operesheni hiyo kuwa washtakiwa.walipambana na wananchi hao uso kwa uso na kufanikiwa kuwapiga risasi wakati wa mapigano, wakati makovu ya risasi hizo kwa watu 10 kati ya 11 walioshtakiwa, yakionyesha kuwa walipigwa upande wa nyuma na kutokea mbele hivyo wapigaji wa risasi hizo hawakuweza kuwaona uso kwa uso.



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form