MAANDAMANO KUIPINGA SERIKALI YAPAMBA MOTO

 Maelfu ya wananchi wanaopinga Serikali wameandamana kwa mara nyingine wakimtaka Rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita kujiuzulu

Licha ya mvua kunyesha, waandamanaji walikusanyika katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Bamako kushinikiza Rais aachie madaraka wakimlaumu kwa masuala mbalimbali ikiwemo ufisadi

Maandamano hayo yamefanyika ni ya kwanza kufanyika tangu Julai baada ya kundi la wapinzani kuingia makubaliano ya muda katika kampeni yao ya kumuondoa Rais Keita madarakani

Hali hiyo imetokea licha ya Rais wa zamani wa Nigeria ambaye pia ni Mpatanishi wa ECOWAS, Goodluck Jonathan kuwasihi wapinzani kuepuka maandamano na kufanya mazungumzo.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form