Kikosi cha Kusini cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kimesema kitafanya msako katika misitu ya mikoa inayopakana na Msumbiji
Kiongozi wa zoezi hilo amewataka wote waliopo katika misitu mikoani Lindi, Mtwara na Ruvuma kuondoka mara moja kupisha operesheni hiyo
Amesema wataanzia Ruvuma na kisha kwenda Lindi kwasababu kuna watu wanaofanya vitendo vya kihalifu ndani ya misitu hiyo
Mwezi Mei mwaka huu Serikali ilisema itapeleka vikosi mpakani kuimarisha usalama kufuatia shambulio lililotokea eneo la Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji.
Tags
BREAKING NEWS