MTOTO KUSAFIRI MPAKA BARUA YA MWENYEKITI

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini, kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 18, anayesafirishwa kutoka eneo moja kwenda jingine anakuwa na kibali cha mzazi na kile cha kiongozi wa serikali za mitaa.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu yaliyohusisha wadau mbalimbali ambapo biashara hiyohufanyika mataifa mbalimbali duniani.

Amebainisha kuwa Wizara itajikita kusimamia safari za ndani ya nchi kwa lengo la kubaini wanaojihusisha na vitendo hivyo ambapo amebainisha kuwa waathirika wakubwa ni wanawake na watoto vitendo ambavyop hutokana sababu mbalimbali ikiwemo tamaa ya pesa na kuibuka kwa soko la vitendovya ngono.

Akizungumzia Watanzania wanaotaka kufanya kazi nje ya nchi amewata kufuata sheria na taratibu zilizowekwa badala ya kuzamia kwa kutumia njia haramu kwa kigezo cha kutafuta maisha akisisitiza kujiridhisha kuhusu kazi husika kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wabinadamu, Amatus Magere katika amesema mapambano hayo wanakabiliwa na changamoto nyingi kwani hufanywa na binadamu wenyewe kwa siri kubwa, kukosekana kwa mfuko wa kusaidia waathirika na upungufu wa raslimali watu.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form