Mahakama ya Rufaa imemuachia huru Amani Justine, aliyekiri kumuua mpenzi wake Gaudencia Mabuli kwa kumchoma kisu baada ya kumtuhumu usaliti
Kwa siku tatu Gaudencia aliripotiwa kupotea na mwili wake uliokotwa barabarani, maeneo ya Vianzi Mei 23, 2012, akiwa na majeraha kwenye bega lake la kushoto, kwenye paji la uso na kiganjani
Askari aliyemkamata Justine, alisema kuwa alimkamata akiwa na T-shirt nyeusi iliyokuwa na damu. Aidha shahidi alisema Marehemu alikuwa na mtuhumiwa siku ya mwisho kabla ya kuripotiwa kupotea
Mtuhumiwa aliomba radhi kwa kusema kuwa ni shetani aliyempelekea kufanya hivyo. Jaji wa Mahakama ya rufaa alisema kisheria ushahidi wa aliyetuhumiwa hautoshi kuhitimisha kuwa ana hatia.
Tags
BREAKING NEWS