UKISIKIA duniani kuna mambo basi malizia kwa kusema ‘tembea ujionee’. Wakati uchimbaji makaburi ikionekana ni kazi ya ajabu hata ikiwa ngumu kuwashawishi vijana wa kileo kujihusisha nayo wapo walioiona kuwa ni fursa kwa kuianzishia mashindano.
Kazi hiyo imeanza kujizolea umaarufu mkubwa katika mataifa mbalimbali ya Ulaya hasa kwa miaka ya hivi karibuni, kutokana na mashindano mbalimbali ya uchimbaji kaburi yanayofanyika.
Kwa kuanzia, hiyo utaipata huko Trencin nchini Slovakia ambako sasa wananchi wake hawashangai kusikia mashindano ya aina hiyo.
Ieleweke kuwa Slovakia si nchi pekee yenye mashindano hayo, kwani itakumbukwa kuwa hata Hungary nayo na lilipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2016, timu 18 zilishiriki mjini Debrecen.
Ni katika shindano hilo ambalo mshindi wake alikwenda Slovakia, jumla ya timu 18 zilishindana huko Hungary, ambapo kigezo kikubwa cha kaburi sahihi ilikuwa ni lenye upana wa futi 2 na inchi 7, urefu wa futi 6 na inchi 6 na kina cha futi 5 na inchi 3