IFAHAMU AMAZON NA JINSI INAVYO FANYA KAZI

 

JEFF BEZOS Mfanya biashara na tajiri namba 1 Duniani, anayemiliki makampuni makubwa kama Amazon, The Washington Post, Blue Origin n.k Leo nimekuletea uzi kuelezea kila kitu kuhusu Jeff Bezos

 

  •  Historia yake na familia yake
  •  Biashara zake na utajiri wake

 


 

              JEFF BEZOS NI NANI ?

           Jeff Bezos ni Mfanya biashara na tajiri namba moja Duniani, ni mwanzilishi na mmliki wa kampuni ya kuuza na kununua bidhaa mtandaoni iitwayo Amazon, anamiliki kampuni ya habari na magazeti "The Washington Post", anamiliki kampuni ya utafiti na utangenazaji wa vifaa vya anga inaitwa "Blue Origin, anamiliki kampuni ya kuuza na kusambaza vyakula inaitwa "Whole Foods" Amepata mafaniko makubwa kupitia biashara zake na kumfanya kuwa Mwanadamu tajiri zaidi Duniani kwa sasa

                   

 

Alizaliwa mwaka 1964 huko New Mexico, Bezos alipenda computer tokea utotoni na alisoma computer science and electrical engineering pale Princeton University, baada ya kumaliza chuo alifanya kazi Wall Street na baadae mwaka 1990 akachaguliwa kuwa senior vice president wa kampuni ya D. E. Shaw Miaka minne baade Bezos aliacha kazi.

                

 

na kuanzisha   http://amazon.com  , ilianza kama kampuni ya kuuza na kununua vitabu mtandaoni na hatimaye leo kila kitu kinauzwa pale

Mwaka 2013 Bezos alinunua The Washington Post na hatimaye 2017 alinunua migahawa maarufu ya Whole Foods ( tutazichambua mbele)

                 

 

 

FAMILIA YAKE JEFF

Jeff Bezos alizaliwa January 12, 1964 huko New Mexico, Mama yake anaitwa Jacklyn Gise na Baba yake anaitwa Ted Jorgensen

Miaka minne baadae wazazi wake walitengana na mama yake aliolewa na Mike Bezos,  hapo ndipo jina la JEFF MIKE BEZOS  limeanzia

                  

 

KUANZISHWA KWA AMAZON

July 16, 1995 Bezos alianzisha http://amazon.com Amazon ni jina linalotokana na mto mrefu huko kusini mwa America, Amazon ilianzia kwenye chumba kimoja na baadae ya mwezi mmoja wakahamia kwenye nyumba yenye vyumba viwili wakiwa na computer 3 tu

                 

 

 

Mafaniko ya Amazon yalikuwa ya kushangaza sana, ndani ya miezi miwili tu waliweza kuuza vitabu ndani ya Marekani na nchi zingine 45 Duniani bila ya matangazo, Mauzo yalifikia $20,000 kwa week ndani ya miezi miwili ya mwanzo, Mwaka 1997 Amazon iliuteka ulimwengu wa digitali.

                         

 

Ambapo wawekezaji walianza kuwekeza na wafanyabiashara mbalimbali walianza kuuza bidhaa zao Amazon,  Mwaka 1998 Jeff alianza kuuza CD,  movies na baadae nguo, electronics  na vingine kupitia mawakala mbalimbali Ikiwa dot.coms za miaka ya '90 zakifilisika lakini Amazon iliendelea kufanya vizuri zaidi na mauzo yaliongezeka kutoka $510,000 mwaka 1995 mpaka $17 billion mwaka 2011 Mpaka mwaka 2018 watu zaidi ya 100 million walikuwa wananufaika na Amazon September 2018 Amazon ilifikia mauzo ya $1 trillion/year ikiwa ni kampuni ya 2 baada ya Apple.

                            

 

kufikia mauzo hayo 2018 Mfanyakazi wa chini Amazon analipwa $15 kwa saa, wenzetu wanalipwa kwa saa Grinning face with smiling eyes

 

 

AMAZON STUDIOS

Mwaka 2013 Jeff Bezos alifungua Amazon Studios, Jeff alisema anaingia rasmi kwenye soko la filamu na burudani ambapo mwaka 2015 watoa filamu yao ya kwanza KINDLE E-READER Mwaka 2007 Amazon waliachia kitu kinaitwa Kindle ( ni kifaa kama tablet) kinamwezesha mtumiaji kununua, Kudownload, kusoma na kutunza vitabu kulingana na chaguo lake Mwaka 2011 Bezos aliingia rasmi kwenye soko la tablet baada ya kuachia.

          

 

Kindle Fire tablet, September mwaka huo walitoa Kindle Fire HD ambayo ni next generation tablet kwa ajili ya kushindana na Apple iPad ‘’We haven't built the best tablet at a certain price. We have built the best tablet at any price," Bezos said, according to ABC News.

                  

 

 

FIRE PHONE

Mwaka 2014 Amazon waliingia rasmi kwenye soko la simu ambapo walitambulisha FIRE PHONE, ni smartphone iliyotengenezwa Amazon Lakini haikufanya vizuri sokoni hivyo Amazon hawakuendelea na utangenazaji wa simu tena

                

 

WHOLE FOODS

Mwaka 2017 Jeff Bezos kupitia Amazon alitangaza kununua migahawa maarufu iitwayo "whole foods" kwa gharama ya $13.7 billion na kuanza rasmi kufanya huduma ya delivery kwa wateja wake kwa mda mfupi zaidi, hali iliyopelekea Walmart na Kroger kuanza kutoka huduma za delivery

UMILIKI WA "The Washington Post"

August 5, 2013 Bezos aliuteka ulimwengu wa habari baada ya kutangaza kununua kampuni la habari na magazeti la "The Washington Post" kwa $ 250 million

 

                      

 

 

 

 UMILIKI WA BLUE ORIGIN

Mwaka 2000 Bezos alianzisha "Blue  Origin" ni kampuni ya utafiti na utangenazaji wa vifaa vya anga, Lego ni watalii kwenda kutalii angani kwa gharama nafuu "Blue Origin" kwa takribani miaka 16 ilifanya kazi kimya kimya na hatimaye mwaka 2016 ilitambulishwa rasmi na sasa inafanya kazi na NASA "He described a vision of humans not only visiting but eventually colonizing space" Miaka 2 baadae walirusha rocket aina ya "Blue Origin Moon Lender" kwa ajili ya Majaribio kupeleka watalii angani kwa mda mfupi.

         

 

UTAJIRI WA JEFF BEZOS

August 2019, Bloomberg na Forbes walikadiria utajiri wake kufikia $ 110 billion na kumfanya kuwa tajiri namba moja Duniani kwa miaka 3 mfululizo

Utajiri wake mkubwa umetokana na Amazon ambapo inakadiriwa mauzo yake ni $260 million kwa siku

              

 

BEZOS EX-WIFE NA WATOTO

Bezos alikutana na Mackenzie Tuttle wote wakifanya kazi D. E. Shaw na hatimaye mwaka 1993 walioana Wote waliacha kazi na kuanzisha amazon, Mackenzie ndiye aliyeandika business plan ya amazon na alifanya kazi kama mhasibu mkuu Walipata watoto wane.

                 


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form