FOMU ZA WABUNGE ZALETA MTAFARUKU



Steven Mengere
maarufu Steve Nyerere ametia nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Msanii huyo amesindikizwa na baadhi ya wasanii wenzake kwenda kuchukua fomu.





Haris Kapiga
Mtangazaji wa Clouds FM na Clouds TV, Harris Kapiga amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge katika Jimbo la Iramba Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).






Fredrick Lowassa
ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge Jimbo la Monduli. Baba yake amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 25 kuanzia 1990 hadi 2015.






Aggrey Mwanri
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro. Mwanri amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo.





Francis Nanai
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea ubunge Jimbo la Kawe.










Mrisho Gambo
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amechukua fomu kwa kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form