RAIS MAGUFULI ALIA NA MIUNDOMBINU

.“Tunatuma fedha za Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) na tunatuma fedha za Halmashauri haiwezekani Barabara mbovu Kusini -DSM, hakuna stendi Somanga, Uchaguzi unakuja, tujipange vizuri na tuchague wawakilishi ambao tutawabana na watatuwakilisha vizuri “Kwa mujibu wa Sheria ya Barabara, Barabara ikishakua ya lami inapata 100% ya ukarabati (Maintanance), Fedha za Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) sijui zinakwenda wapi!, Serikali haijalala, hili la ubovu wa Barabara (Kusini-DSM) nawahakikishia nitalishughulikia mwenyewe”. “Kazi aliyoifanya Mkapa ameifanya kwa nguvu zote, nawaomba wananchi wa kusini tumuenzi Mkapa kwa kuchapa kazi, tuna eneo zuri mno, ufuta unakubali, mahindi, korosho vyote vinakubali, na mifugo inakubali, tuchape kazi na tupendane, Kero ya Barabara (Kusini-DSM) hii nimeibeba” “Barabara hii ya Mtwara - Lindi-Dar es salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange vizuri utunzaji sio mzuri”-JPM njiani kuelekea DSM ,Ilibidi niende Dar es Salaam kwa kutumia Ndege kutokea Mtwara lakini nimepita hii Barabara (Mtwara- DSM) makusudi nione hali yake, hii Barabara imeharibika, 90 KM zote zimeharibika. magari yenye uzito mkubwa yameharibu hii Barabara”-JPM njiani kuelekea DSM


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form