ACT Wazalendo tukiingia Ikulu October 2020.
1. Tutashughulikia kwa ukamilifu tatizo la ajira kwa vijana na wale wahitimu wa vyuo vikuu ambao wapo vijiweni bila kazi.
2. Suala la mishahara ya watumishi wa vyombo vya usalama litapata kipaumbele.
Tutapandisha mishahara ya wafanyakazi wote ambao kwa kipindi chote cha miaka mitano hawajapata nyongeza za mishahara na promotion.
3.Kwenye utawala wetu tutapanua wigo wa demokrasia, Uhuru na kuheshimu haki za binadamu.
Hamtasikia tena kuwa kuna udukuzi au watu wasiojulikana.
Hukutakuwa na hofu ya kutekwa, kutumbuliwa wala hofu ya kupoteza uhai kwenye utawala wetu.
4. Tutajenga mazingira mazuri tena kwa ajili ya kuvutia wawekezaji. 5. Tutaimarisha sekta ya kilimo.
6. Tutaimarisha sekta binafsi iwe kweli engine ya maendeleo ya uchumi wetu.
7. Tutaimarisha Economic Diplomacy na kurejesha mahusiano ya kimataifa ambayo yameathirika vibaya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
8. Tutawaheshimu, tutawatendea haki na tutawapa moyo wafanyabiashara na ikiwezekana kuwarudisha wote walioihama nchi.Wafanyabiashara siyo maadui wa Serekali bali ni marafiki.
9. Serikali yetu itaheshimu utawala wa sheria, na itaanzisha tena mchakato wa katiba mpya.
10. Bei za mazao ya Pamba, Korosho, Ufuta, Alizeti, Mbaazi zitatafutiwa masoko ya kuaminika ili wakulima wapate kuuza mazao yao.
11. Bagamoyo Port expansion itapewa kipaumbele.
12. Mradi wa Gasi ya Lindi/Mtwara- Utapata kipaumbele.
13.Bureu du Change zote tutazirudisha na madai yote halali ya wafanyabiashara wa maduka ya kubadilisha fedha yatashughulikiwa na kulipwa.
Tags
BREAKING NEWS