TENDO LA NDOA LAMPELEKA KUZIMU

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Dalali Malongo (20) Mkazi wa Kijiji cha Mipanga Kata ya Maji Moto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na mume wake aitwaye, Kisabo Joseph baaada ya mume wake kukasirishwa na kitendo cha mke wake kumnyima tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga tukio hilo la mauaji ya kikatili na ya kusikitisha lilitokea Julai 14, mwaka huu majira ya saa moja jioni huko katika Kijiji cha Mipanga Kata ya Maji Moto Wilaya ya Mlele.

Amesema,marehemu na mtuhumiwa walikuwa ni wanandoa waliokuwa wakiishi pamoja kama mume na mke,lakini katika ndoa yao inasemekana marehemu alikuwa akikataa kufanya tendo la ndoa pindi mume wake alipokuwa akihitaji kupatiwa tendo la ndoa na mke wake.

Hali ambayo inasadikiwa kuwa marehemu huenda alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine ambaye alikuwa akifanya nae tendo la ndoa na kumnyima mume wake tendo hilo.

Amesema, hali hiyo imemfanya mume wa marehemu achukie, hivyo siku ya tukio mume wa marehemu alimvizia marehemu wakati akienda kutaka maji kwenye chanzo cha Maji ya Moto

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form