Mwili wa Rais Benjamin Mkapa unasafirishwa mchana leo kuelekea mkoani Mtwara ambapo utapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Masasi na kisha kupelekwa nyumbani kwake Kijiji cha Lupaso, mkoani humo. Mwili huo unasafirishwa baada ya kumalizika kwa shughuli za kuuaga Dar es Salaam.