Msemaji wa Familia ya Mkapa, William Erio amesema Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alifariki kutokana na mshituko wa moyo. Erio amesema kiongozi huyo alikuwa amelazwa baada ya kuugua Malaria lakini vipimo vya mwisho vinaonesha alipata mshtuko wa moyo wakati akisimama kutoka kitandani.