Brian Deacon alizaliwa tarehe 13/2/1949, Oxford nchini Uingereza. Alipata mafunzo ya uigizaji katika jumba la sinema la Oxford Youth Theatre ambapo walikuwa wakifanya maigizo ya jukwaani.
Mwaka 1979 Taasisi ya kiinjilisti ilitaka kutengeneza movie ili kuonyesha maisha aliyoyaishi Yesu ambayo yameandikwa kwenye injili ya luka. Mtayarishaji wa filamu hii bwana John Heyman alipeleka wazo hili Hollywood ili waweze kuwawezesha lakini Hollywood waligoma kuwawezesha
Baadae Taasisi ya Campus Crusade ili wawezesha takribani kiasi cha $ 6 million ili kufanikisha project hiyo, Filamu hii ilihusisha washiriki zaidi ya 5000 lakini maarufu zaidi ni bwana Brian Deacon aliyecheza kama Yesu. Waliitisha mchujo ambapo watu zaidi ya 1000
walijitokeza kuwania nafasi ya kucheza kama Yesu lakini Brian Deacon aliweza kushinda nafasi hiyo. Ili kuweza kuwasilisha vizuri mafundisho ya Yesu Brian Deacon alikuwa anasoma biblia has a kitabu cha luka zaidi ya mara 20 kabla hajaanza kushoot ili kufikisha ujumbe sahihi kwa watazamaji watakaotazama movie hiyo
Alifuga nywele na ndevu lakini mtayarishaji alipendelea bwana Deacon atumie wigi ili kuwa na muonekano halisi wa kizamani. Iliwachukua miezi saba mpaka kumaliza kushoot movie hiyo huku wakipitia mikasa mingi likiwemo la kuungua kwa hoteli
waliyofikia huko Tel Aviv, tukio lililotokea usiku mzito lakini walifanikiwa kutoka wakiwa salama na kesho yake waliendelea na kazi yao ya kushoot kama kawaida, baadhi ya washiriki kugoma kutokana na malipo kidogo lakini walifanikisha kushoot movie nzima wakiwa salama
Movie nyingine alizocheza ukiacha hii ya yesu ni pamoja na Tha Feathered Serpent, A zed & Two Noughts, Brian Deacon alifanikiwa kufunga ndoa na mwanadada Rula Lenska mwaka 1977 na kufikia mwaka 1987 waliachana na alifanikiwa kuoa tena mwaka 1998 ambapo alimuoa Natalie Bloch ambaye wanaishi wote mpaka sasa
=========================================================================
Brian Deacon was born on 13/2/1949, Oxford in the United Kingdom. He received acting training at the Oxford Youth Theater where they were performing on stage.
In 1979 the Evangelical Institute wanted to make a movie to show the life of Jesus which is recorded in the gospel of Luke. The producer of this film Mr. John Heyman sent this idea to Hollywood so that they could empower them but Hollywood refused to empower them
Later on the Campus Crusade Institute to raise about $ 6 million to make the project a success, the film involved more than 5000 participants but the most famous is Mr. Brian Deacon who played as Jesus. They called for a selection where more than 1000 people
they competed for the role of Jesus but Brian Deacon won the title. In order to better present the teachings of Jesus Brian Deacon was reading the bible has a book of Luke more than 20 times before he started shooting to convey the right message to the audience who will watch the movie
He grew hair and a beard but the producer preferred Mr. Deacon to use a wig to have a more outdated look. It took them seven months to finish shooting the movie as they went through many tragedies including the burning of a hotel
they arrived in Tel Aviv, an incident that took place overnight but they managed to get out safely and the next day they continued their shooting work as usual, some participants went on strike due to low pay but managed to shoot the whole movie safely
Other movies he has played besides Jesus include Tha Feathered Serpent, A zed & Two Noughts, Brian Deacon successfully married Rula Lenska in 1977 and in 1987 they divorced and he remarried in 1998 where he married Natalie Bloch who they both live until now