BABA ASHINDWA KUOA BAADA YA KIJANA WAKE KUTOROKA NA MAHARI

Mvulana mwenye umri wa miaka 17 katika Kaunti ya Tana River, nchini Kenya ametorosha mahari iliyokusudiwa kutumiwa na baba yake mwenye umri wa miaka 74 kuoa mke wa nne, na amewaelezea wazee kwamba msichana aliyetaka kumuoa alikuwa mchumba wake, ndio maana alichukua hatua hiyo.

Mvulana huyo ambaye alirudi nyumbani Jumapili baada ya kushawishiwa na vijana waliotumwa kumsaka vichakani, alikotorokea na ng’ombe waliokuwa watumiwe kulipa mahari, alisema alifanya hivyo baada ya juhudi zake za kuwashawishi wazee kumzuia baba yake asimuoe mchumba wake kugonga mwamba.

Mzee mmoja aliyengoza mchakato wa upatanishi, alisema sababu kubwa ya kijana huyo kupinga baba yake kufanya hivyo ni kuwa msichana tayari ana mimba yake ya miezi mitatu.

Alisema “msichana huyo alikuwa aozwe kwa mzee huyo ili kuepusha aibu kwa familia yake, baada ya wazazi kugundua alikuwa mjamzito nje ya ndoa na hakutaka kumtaja aliyehusika” .

Kijana alisema waliamua kupata ujauzito na mchumba wake kama njia ya kumshawishi baba yake akubali waoane, akidai baba yake alikuwa na tabia ya kukataa wachumba wake wote.

======================================

A 17-year-old boy in Kenya's Tana River County has escaped a dowry intended to be used by his 74-year-old father to marry a fourth wife, and he has told elders that the girl he wanted to marry was his fiancé, which is why he took the initiative.

The boy, who returned home on Sunday after being persuaded by young men sent to look for him in the bushes, escaped with cattle used to pay dowries, said he did so after his efforts to persuade the elders to prevent his father from marrying his fiancée hit a rock.

An elder who led the mediation process, said the main reason for the boy's refusal to do so was that the girl was already three months pregnant.

He said "the girl was to be married to the old man to avoid embarrassment to her family, after the parents found out she was pregnant out of wedlock and did not want to name who was responsible".

The young man said they decided to get pregnant with his fiancée as a way to persuade his father to agree to marry them, claiming his father had a habit of rejecting all his fiancées.





Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form