Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Charles amewaagiza wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Dkt.Charles ametoa agizo hilo wakati anafungua mafunzo ya uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo Kanda ya Ruvuma yenye mikoa ya Njombe, Ruvuma,Mtwara,Lindi,Iringa na Mbeya.Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
“Kama unavyoona Taifa letu sasa hivi kuna baadhi watu wanachokochoko sana,kwa hiyo mjitahidi kufanya kazi kwa kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka shari ya watu hao’’,alisisitiza Dkt.Charles.
Amesema hadi sasa NEC imeshatuma sehemu kubwa ya vifaa vya kufanikisha uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu na kwamba vifaa hivyo vimekwishaanza kusambazwa na inatarajiwa hadi kufikia Oktoba 24 kila Halmashauri nchini itakuwa imepokea vifaa vyote vya uchaguzi.
Amewashauri wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo kuanza kuvipakua vifaa hivyo na kuvisambaza katika maeneo yote na kwamba wasisubiri hadi Oktoba 27.
“NEC katika uchaguzi wa mwaka huu tunataka kuwa tofauti ukilinganisha na mwaka 2015,kwanza serikali imetuletea fedha zilizotokana na kodi za walipa kodi kwa wakati,hivi tunavyoongea zaidi ya shilingi bilioni 120 nimezishusha ngazi ya Halmashauri’’,alisisitiza Dkt.Charles.
Amewataka wasimamizi hao kufikisha vifaa vya uchaguzi ngazi ya Kata kwa wakati ili wale ambao wamezoea kulalamika kuwa NEC imechelewa kufungua vituo na kuchelewesha vifaa katika uchaguzi wa mwaka huu wakose cha kusema.
Kwa mujibu wa Dkt. Charles,kuanzia Oktoba 24 hadi 26 NEC itaanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.
======================================
Director of Elections Dr. Wilson Charles has instructed state-level election officials to carry out their duties in accordance with the law to avoid complaints that could lead to breaches of the peace.
Dr. Charles issued the order while opening the election training for the election administrators of the Ruvuma Zone constituencies consisting of Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Iringa and Mbeya regions. The training was held at the Songea Municipal Hall.
"As you can see in our nation right now there are some people who are very provocative, so try to work on the rules and regulations of the election to avoid the evil of those people," stressed Dr. Charles.
He said so far the NEC has sent a large portion of equipment to win the general election which is expected to take place on October 28 this year and that the equipment has already been distributed and it is expected that by October 24 each council in the country will have received all election materials.
He advised state election officials to start downloading the materials and distributing them in all areas and not to wait until October 27.
"NEC in this year's elections we want to be different compared to 2015, first the government has brought us the money from taxpayers' taxes on time, as we speak more than 120 billion shillings I have lowered the level of Council", stressed Dr. Charles.
He urged the supervisors to deliver the election materials to the ward level on time so that those who are accustomed to complaining that the NEC has been late in opening polling stations and delaying the materials in this year's elections have nothing to say.
According to Dr. Charles, from October 24 to 26 NEC will begin training election officials.