Wanafunzi 36 wa shule ya wasichana ya Mtakatifu Joseph iliyopo jijini Mwanza wamenusurika kifo baada ya bweni moja la shule hiyo kuungua moto na kusababisha hasara ya mali na vitu mbalimbali vya wanafunzi.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Florida Busasi amesema tukio hilo la moto limetokea majira ya saa 11 alfajiri ya Julai 23 kwenye bweni lenye vyumba vitatu vyenye uwezo wa kuchukua itvitanda 18 ambapo wanafunzi hao wamepoteza kila kitu zaidi ya kubaki na nguo walizokuwa wamevaa .
Tags
BREAKING NEWS