Bunge la Uturuki limepitisha Sheria ya kusimamia maudhui ya mtandaoni, hatua ambayo wakosoaji wanadai itaongeza udhibiti na kusaidia Mamlaka kuficha mawazo tofauti na yale waliyokuwa nayo
Makampuni ya nje yakiwemo Facebook na Twitter yatatakiwa kuwa na Wawakilishi nchini humo ili kushughulikia malalamiko kuhusu maudhui yaliyopo katika mitandao yao
Mitandao itakaoshindwa kufanya hivyo itapunguziwa uwezo wa kufanya kazi, itatozwa faini na kuzuiwa kujitangaza. Pia, faini zitatozwa ikiwa maudhui yasiyokubalika hayataondolewa ndani ya saa 24
Waturuki wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali mtandaoni na baadhi wamefunguliwa mashtaka kwa kumtukana Rais Recep Tayyip Erdogan au Mawaziri wake huku wengine wakishtakiwa kwa kukosoa namna janga la COVID19 linavyoshughulikiwa
Tags
BREAKING NEWS