Makanisa mengi Kenya yamejikuta yakipata idadi ndogo ya waumini tangu Serikali iondoe marufuku ya mikusanyiko ya kidini
Idadi kubwa ya waumini wameamua kufuatilia ibada za makanisa yao kupitia mtandao huku makanisa yakipata waumini wasiozidi 100
Kanisa la PEFA lililopo Migori lilipata waumini 140 katika ibada nne huku makanisa mengine yakiwemo Citam Kisumu na ACK Dago yakiendelea kufungwa
Padri Bernard Juma wa Kanisa la Anglikana la Kenya (ACK) Parokia ya Makongeni, Homa Bay ametoa wito kwa Serikali ya Kaunti hiyo kuwaisaidia kununua vipima joto na kuwaomba watu kuchangia vitakasa mikono
Amesema baadhi ya makanisa yanapata wakati mgumu kwasababu ya gharama kubwa ambazo Wakristo wengi hawawezi kumudu
We
Tags
BREAKING NEWS