Mwanamuziki Zena Mohammed maarufu Shilole ametangaza kuachana na mume wake, Uchebe, kwa sababu amekuwa akimpiga mara kwa mara bila sababu za msingi. Aidha, ameomba radhi kwa kuuaminisha umma kuwa ndoa yake haikuwa na matatizo huku akificha ukweli kuwa alikuwa akipigwa na mumewe.