WANANCHI WA MALI WAMSURUBU RAIS WAO

Viongozi wa upinzani nchini Mali wamemtaka rais Ibrahim Boubacar Keita kujiuzulu , baada ya kukataa makubaliano yaliolenga kuzuia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Takriban watu wanne waliuawa wakati wa maandamano siku ya Ijumaa , na kulikuwa na makabiliano zaidi siku ya Jumamosi.

Maandamano hayo yalimlazimu rais kufutilia mbali mahakama kuu ambayo imekuwa katikati ya mgogoro huo baada ya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi mwezi Machi.

Lakini muungano wa upinzani ulikataa pendekezo lake muda mfupi baadaye.

Nouhoum Togo, msemaji wa kundi la M5-RFP la viongozi wa kidini pamoja na wanasiasa ambalo liliandaa maandamano ya hivi majuzi amesema kwamba 'hatuwezi kukubali upuzi huu'.

''Tunataka ajiuzulu mara moja'' , aliambia chombo cha Reuters siku ya Jumapili.

Wapinzani hawafurahii jinsi rais Keita anavyolisimamia suala la wapiganaji wa Kijihad, mzozo wa kiuchumi na uchaguzi huo ambayo matokeo yake yanapangwa.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form