"Oktoba 13 jiji letu (Dar es Salaam) lilipata mvua kubwa na kuleta athari ikiwemo vifo 12, nyumba 800 zilizingirwa na maji, nyumba 107 zimechukuliwa na maji, na Wananchi 480 wamekosa mahali pa kukaa, maeneo yaliyoathirika ni Kisutu,Tupendane,Barafu, Kisiwani nk" RC Kunenge.
"Serikali itajenga Daraja Jangwani na kuboresha Mto Msimbazi, ile changamoto ikinyesha mvua hatupiti Jangwani itapata jibu. Eneo lile la Dawasa Tegeta na maeneo jirani kuna changamoto ya maji pia itajengwa mifereji ya chini kupeleka maji Baharini" RC Kunenge.
Tags
BREAKING NEWS