Watu watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha daladala na lori la mchanga katika eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amesema chanzo cha ajali iliyotokea asubuhi ya leo Oktoba 5, 2020 eneo la Chang’ombe kati ya Daladala na lori la mchanga ni mwendo kasi wa daladala na kwamba dereva wake amekimbia na polisi inaendelea kumtafuta.
Tags
BREAKING NEWS