Msimamizi wa uchaguzi katika majimbo ya Moshi Mjini, Moshi Vijijini na Vunjo, Michael Mwandezi, amewataka wananchi wote wanaofika kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za wagombea kuondoka katika viwanja vya kampeni baada ya kutimia saa 12 jioni ili kutii sheria za uchaguzi.
"Kwa mujibu wa maelekezo ya Tume ya Uchaguzi kwa vyama vya siasa na wagombea ya mwaka 2020, mgombea au chama chake hakipaswi kubandika mabango kwenye eneo la mtu binafsi bila ridhaa yake"Michael Mwandezi, Msimamizi uchaguzi majimbo matatu ya Moshi Mjini, Vunjo na Moshi Vijijini
"Ikitokea mgombea amepitiliza muda wa kampeni wa saa 12:00 jioni, itahesabika ni kuvunja sheria na kusanyiko lolote baada ya muda huo halitahesabika kama ni mkutano wa kampeni, ni kosa kisheria"Michael Mwandezi, Msimamizi wa uchaguzi majimbo ya Moshi Mjini,Moshi Vijijini na Vunjo
