Rais wa Tanzania football, Wallace Karia amesema uamuzi wa kupunguza timu ligi kuu soka Tanzania bara, ulitokana na maoni ya wadhamini na wadau wakiwemo waandishi wa habari, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa mashindano. Msimu huu zimeshiriki timu 18 na msimu ujao zitakuwa timu 16.
"Ni kweli Viwanja vingi vipo kwenye hali mbaya sana kutokana na baadhi ya shughuli ambazo zinafanyika ni za kiharibifu, tunakaribia kuingia mkataba na wamiliki tushirikiane kufanya ukarabati kwa ajili ya kutatua tatizo hilo" Wallace Karia Rais wa Tanzania football
"Tumeiomba Serikali shughuli za matamasha zifanyike nje ya viwanja maana matamasha yanaharibu sana viwanja, hatuiogopi kuiambia Serikali ila tunashirikiana nao kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa viwanja hivyo, tusipokaa nao hatufiki popote" Karia
"Kwa asilimia kubwa Tanzania hatuna maafisa wa habari tuna wahamasishaji, watu wanaongea vitu kutoka kichwani mwao, Afisa Habari anatakiwa kutoa taarifa zilizotolewa na taasisi, kwetu tuna hiyo changamoto, sasa tunaandaa miongozo" Karia.
"Kuna timu zingine zinapanda Ligi Kuu zinataka kushindana na SimbaSCTanzania au Yang kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni, ikishafika huko bajeti zao zinapanda wanajikuta wanakwama" Wallace Karia.
"Wachezaji wetu wa Tanzania wanacheza muda mfupi kutokana na matatizo ya viwanja ambapo majeraha yanawaondoa mapema kwenye michezo" Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
"Tumewaambia namungo fc katika michuano ya kimataifa waje kuchezea Dar Es Salaam, uwanja wao haujakidhi kimataifa CAF wakija kuukagua watakwama, nadhani watatuelewa ingawa wao wameng'ang'ania kwenye uwanja wao" Wallace Karia.






