KAMATI YA MAADILI YAPIGILIA MSUMARI ADHABU YA TUNDU LISSU

Kamati ya Madili ya Kitaifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepigilia msumari wa mwisho kuwa adhabu iliyotolewa na kamati hiyo kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.Tundu Lissu ni sahihi na kuongeza kuwa, haruhusiwi kupanda kwenye jukwaa lolote la siasa hadi adhabu hiyo iishe



"Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni, atambue kuwa kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa"- Emmanuel Kawishe, Katibu wa Kamati ya Maadili ya Kitaifa 



"Tume haimpelekei taarifa mgombea mmoja mmoja, taarifa inapelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyao, hivyo madai ya Tundualissu kuwa hajapokea taarifa ni uongo"- Emmanuel Kawishe, Katibu wa Kamati ya Maadili ya Kitaifa.



"Adhabu inatakiwa kutekelezwa kwa kuwa imetolewa na chombo chenye mamlaka ya kisheria na kwa kuzingatia utaratibu, mgombea urais wa CHADEMA Mhe. Tundu Lissu anatakiwa kuheshimu na kutekeleza adhabu hiyo kama ilivyotolewa"- Emmanuel Kawishe




"Suala la Tundu lissu limetangazwa kwa sababu ni sehemu ya adhabu aliyopewa na kamati, Kamati siyo Tume ya uchaguzi bali ni chombo kinachoundwa na vyama vyote vyenye wagombea wa kiti cha rais"- Emmanuel Kawishe, Katibu wa Kamati ya Maadili


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form