Katibu Muenezi wa CCM, Humohrey Polepole amesema upinzani huwa hauongezeki, ukiona kitakwimu umeongezeka huwa inakuwa ni matokeo ya CCM wakiwa na mgogoro wa ndani
CCM wakiwa na mgogoro wa ndani ndio huamia vyama vingine kitu ambacho hufanya takwimu zioneshe kuwa upinzani umeongezeka
Anasema kwa awamu hii ya Dkt. Magufuli hakukuwa na nafasi ya kuwa na mgogoro wa ndani ya CCM , ndiyo maana mwaka huu 2020 upinzani haujaweza kuongezeka
Aliyasema hayo akiwa anajibu maswali ya Waandishi wa Habari alipokuwa akizungumza nao Zanzibar, Jana
Tags
UCHAGUZI