:SIMULIZI-MUUAJI MWENYE ROHO YA HURUMA-01
MTUNZI-ANDREW SHADU
EMAIL-andrewshadu44@gmail.com
>>>MWANZO>>>
Jiji la Dar es salaam ni jiji dogo sana ukilinganisha na majiji mengine kama vile Mwanza na Mbeya lakini jiji hilo la Dar es salaam limetokea kujipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na matukio mengi ya kibiashara ambayo yanafanyika ndani ya hilo. Mji huo wa Dar es salaam ni mji mdogo sana lakini matukio yanayotokea ndani ya huo mji ni matukio makubwa kuliko hadi ukubwa wa mji huo. Watu wengi waishio mikoani huwa wanakuwa na ndoto ya kuingia kwenye jiji la Dar es salaam lakini wakifanikiwa kufika huwa wanaambulia kufaidi uzuri wa magorofa yaliyo posta kisha wanageuza kurudi mikoani kwao walipotoka kwasababu maisha ndani ya jiji la Dar es salaam yanakuwa ni magumu sana kwa upande wao kuliko hata walivyokuwa wanawaza kabla ya kufika Dar es salaam. Ilikuwa ni Jumanne mida ya saa nane mchana jua likiwa kali sana, Wananchi wengi waliokuwa wamekusanyika kwenye viunga vya maeneo ya Tandika walionekana kuchukizwa na lile jua ambalo lilikuwa linawakomoa, kwani lilikuwa linawachoma vilivyo kwenye vichwa vyao, Watu wengi walionekana kununua mahitaji yao kwenye soko la Tandika huku wakilalamika sana kuhusu ukali wa jua. Hakukuwa hata na Tone la mvua lakini miamvuli ilipata sana soko kwasababu watu walionekana kuigombania kwa ajili ya kujikinga na jua ambalo liliwafanya wawe wanatokwa na jasho kwa wingi..."aisee hizi ni dalili kabisa za mwisho, mbona leo jua limekuwa kali hivi kama limeshushwa jamani"...alisikaka mwanamama mmoja akilalamika huku akiendelea kuchagua aina ya gauni ambalo alikuwa anataka kulinunua..."Binadamu bana hamnaga shukurani hata kidogo, ikinyesha mvua mnalalamika, lilikipa jua mnalalamika"...Kijana mmoja aliyekuwa anachagua viatu vya mtumba kwa pembeni alimjibu yule mama na kusababisha Tafrani itokee kwenye lile soko la Tandika, yule mama alikuwa ana mdomo mchafu sana kwani alianza kumtukana yule kaka wa watu bila huruma, Ilifikia hatua akaanza kutukana na matusi ya nguoni kabisa. Mwanzoni yule kaka alikuwa amenyamaza huku akiendelea na mambo yake lakini alivyoona yule mama anazidi kumdharirisha, Aliamua kumkunja kisha akamchapa kibao kikali kilichomfanya yule mama aangukie kwenye bidhaa za watu wengine...."Wewe mama nitakuua ujue, usijaribu tena kunitukania mama yangu hata mara moja"...aliongea yule kijana huku akiwa anahema juu juu kwa hasira. Mwanamke ni kiumbe mwenye uahawishi mkubwa sana mbele ya jamii, mwanamke pia anaweza akakuua kwa dakika chache kwani yule mama baada ya kuanguka chini kitu cha kwanza kilichokuja akilini mwake ni kupiga kelel e ya mwizi ili kumkomesha yule kijana asiye na kosa..."Mwiziiiiiii, jamaniii mwiziiiii, mwiziiiiii"...Ni kelele za yule mama zilivyosikika vizuri kwa watu wa karibu na lile tukio ambao hawakujua chanzo cha ule ugomvi ni nini. Haikupita muda mrefu lilifumuka kundi la vijana wakiwa wameshikilia magongo huku wakija kwenye uelekeo wa yule kijana ambaye naye aliona njia sahihi ni kukimbia ili kuiokoa nafsi yake ambayo ilikuwa hatiani. Yule kijana alikimbia sana lakini kama ujuavyo wingi wa soko la Tandika basi kila mahala alipokuwa anakatiza alikuwa anakutana na watu waliokuwa wameshikilia silaha kwa lengo la kumdhuru, Yule kijana hakufika mbali alitandikwa gongo la mkono na mtu mmoja hadi akayumba, Hakukaa vizuri lilitupwa tofali kubwa linakwa linakuja kwenye maeneo ya kichwa chake lakini kwa bahati mzuri aliwahi kuinuka akaingia kwenye kichochoro kidogo ambacho alikifatisha na kutokeza ndani ya duka la nguo za wanawake. Yule kijana alivyofika ndani ya lile duka alipitiliza moja kwa moja hadi kwenye masanduku ya nguo nakujificha huku akihema sana. Muuzaji wa lile duka alikuwa ni mdada mwenye hasiri ya kihindi ambaye alimshuhudia yule kijana pindi alipokuwa anaingia dukani mwake, Yule dada aliingiwa na wasiwasi akawa anajiandanaa kwenda kumchunguza yule kijana aliyeingia kujificha kwenye masanduko ya nguo. Yule mwanadada mwenye asili ya kihindi kabla hajafanya chochote alishtukia kundi kubwa la watu likiwasili kwenye duka lake huku likiwa limeshikilia silaha mbali mbali, wengine walikuwa wamebeba mawe, wengine wamebeba magongo, wengine matofali..."Oya wewe dada kama kuna boya kaingia humundukani mwako tutolee haraka, tunamtamani kichizi huyo mwizi, kitambo ujue hatujaua"...aliongea Teja mmoja aliyekuwa anaongea huku udenda ukimtililika mdomoni. Yule dada alitaka kumtaja yule kijana kuwa amejificha ndani ya duka lake lakini alisita kwani hakuwa tayari kuona mtu akiuliwa mbele ya duka lake..."hapana hajani, mimi sijamuona mtu yoyote kwakweli"...alijibu yule dada huku akiwa mwingi wa wasiwasi..."Oya wadau achaneni na huyu manzi anatupotezea muda, yule boya lazima atakuwa mitaa ya karibu na eneo hili, kama vipi tukamcheki maduka ya mbele pale"...aliongea yule teja kisha lile kundi likaelekea kwa mbele. Masikini yule dada mwenye asili ya kihindi alivuta pumzi kwa nguvu baada ya wale watu waliokuwa wanamtafuta mwizi wao kuishia. Yule dada ilibidi aelekee moja kwa moja hadi kwenye yale masanduku ya nguo huku akiwa na wasiwasi kwani hata yeye alikuwa anamuogopa yule kijana ambaye aliingia kwenye duka lake kujificha..."Wewe kaka haya ondoka haraka, sitaki kushuhudia mauaji kwenye duka langu"...aliongea yule dada akimsihi yule kijana aondoke..."nisaidia dada yangu nitauliwa bule, sijamuibia mtu yoyote bali wanataka kuniua bule, nimesingiziwa kuiba dada yangu"...yule kijana aliongea huku machozi yakimtoka kwani alikuwa anahisi maumivu kwasababu ule mkono aliopigwa na gongo ulikuwa unavuja damu. Yule dada mwenye asili ya kihindi aliingiwa na huruma juu ya yule kijana kwani aliamua kuchukua madawa yao ya kihindi kisha akaanza kumpaka kwenye ule mkono ulioumizwa, baada ya muda mfupi damu zilikata na maumivu yakapungua..."unaitwa nani"...aliuliza yule dada..."naitwa Ziko"...alijibu yule kijana ambaye kwa wakati huo alimshukuru sana yule dada na kumuona kama ndiye mkombozi wa maisha yake kwa siku iyo..." okay Ziko inabidi ujifiche apo apo hadi ikifika usiku ndiyo uondoke zako kwasababu ukiondoka muda huu wanaweza kukuona na kukudhuru"...aliongea yule dada kisha akawa anaendelea na shughuri zake. Usiku wa saa nne ulivyofika yule kijana aliyejulikana kwa jina la Ziko alijiandaa kwa ajili ya kurudi sehemu aliyokuwa anaishi lakini walivyotoka tu ndani ya lile duka akiwa na yule dada mwenye asili ya kihindi waliweza kukutana na yule teja wa mara ya kwanza uso kwa uso.
Usikose muendelezo.