BARAZA LA MITIHANI TAIFA LATANGAZA MITIHANI YA DARASA LA SABA KUANZA HAPO KESHO

Dkt Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ametangaza kuwa kuanzia kesho Oktoba 7 hadi 8, 2020, wanafunzi wa darasa la saba watafanya mitihani ya Taifa ya kumaliza elimu ya msingi kwa Tanzania Bara na visiwani Zanzibar.


"Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa, kufanya kazi yao kwa uadilifu wa hali ya juu na wahakikishe wanalinda haki ya watahiniwa wenye mahitaji maalum"- Katibu Mtendaji NECTA, Dkt. Charles Msonde.


"Baraza linawataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani" - Katibu Mtendaji NECTA, Dkt. Charles Msonde.









Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form