Klabu ya PSG imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo, Danilo Pereira kutoka klabu ya FC Porto kwa mkopo wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja mara baada ya muda wake wa mkopo utakapo malizika.
Klabu ya PSG imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Everton, Moise Kean kwa mkopo wa mwaka mmoja. Kean (20) alijiunga na Everton msimu uliopita akitokea Juventus, amefunga magoli manne kwenye mechi 37 alizocheza kwenye mashindano yote akiwa na Everton.
Klabu ya AC Milan imethibitisha kukamilisha usajili wa beki Diogo Dalot kutoka Manchester United kwa mkopo. Dalot mwenye umri wa miaka 21 amechagua kuvaa jezi namba 5.
Tags
SPORTS