Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera amesema ifike wakati Afrika ifanye chaguzi zake kwa kujitegemea wenyewe bila kualika waangalizi kutoka nje ya bara hilo. Amesema mara nyingi waangalizi wanaokuja Afrika huandika yale wanayoyataka wao, na wakati mwingine huwa si sahihi.
“Lazima tufanye Chaguzi zetu bila Waangalizi wa Kimataifa kwasababu wao wakija huwa wanatoa taarifa zao wenyewe wanazoamua kuzitoa, Afrika inaweza kuimairisha Demokrasia yake yenyewe, tuchukue jukumu letu na sio kusubiri wengine”-Chakwera mbele ya JPM
Tags
BREAKING NEWS