ALI KIBA AOMBA MWALIMU NYERERE ATENGENEZEWE ‘DOCUMENTARY’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba amemuomba Rais Magufuli atenge bajeti ya fedha zitakazotumika kutengeneza ‘documentary’ ya maisha ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Amesema ikitengenezwa itakuwa na faida mbili, ikiwemo kufanya Nyerere azidi kukumbwa na kufahamika kwa vijana ambao wamezaliwa baada ya kifo cha Nyerere.


Aidha amesema itasaidia kuwainua wasanii wa maigizo nchini ambao wamekuwa wakishirikiana nao kwenye majukumu mbalimbali ya kujenga taifa.


Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni Rais wa kwanza wa Tanzania, muasisi wa taifa na mpigania uhuru aliyefariki Oktoba 14, 1999.



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form