TULIA AKSON ATOA SIRI YA MAFANIKIO BAADA YA UCHAGUZI

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson ameendelea na ziara zake za kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu wa October 28, 2020 ambapo leo alikuwa katika kata ya Uyole Jijini humo akiwaeleza Wananchi sababu za kukichagua chama chake ili kujipatia maendeleo ya kasi zaidi.


“Safari hii Mbeya mjini propaganda zilizoganda tunasukuma nje, kama mtu hakufanya kazi kwa miaka kumi safari hii chagueni CCM mjionee mafanikio ya haraka, CCM tumejipanga kwa ajili ya maendeleo hapa Mbeya mjini na leo nitawaeleza machache tu ambayo tumekwishayafanya na tutayafanya zaidi endapo mtatuchagua kuwatumikia”- Dr. Tulia Ackson


“Tega sikio mwana-Uyole nikueleze kwamba nikianza kwa hapa shule yetu ya msingi Uyole mimi Mbunge wenu wa kujiongeza nimeshapeleka pale madawati hamsini ambayo ni zaidi ya Shilingi milioni nne na laki tano, tukisema safari hii Mbeya mjini tunachagua Mbunge wa kujiongeza basi mjue huko ndio kujiongeza. Sikuwa na mfuko wa Jimbo lakini mmeyaona niliyoyafanya”- Dr. Tulia Ackson


“Mtaa wetu wa Hasanga hapo Shule ya Hasanga changamoto zao nazijua na nikisema nitazishughulikia ni kwasababu kazi imeanza, kwahiyo hata shule ya msingi Kilimo tutaifikia kwasababu sisi ni watu wa kazi sio manenomaneno. Shule yetu ya Sekondari Pankumbi tumeshapeleka pale mabati 100 ambayo gharama zake ni karibu Milion mbili na laki saba, tumepeleka mifuko 100 ya cement sasa ndugu zangu nawaeleza kwamba tupo vizuri na tumejipanga”- Dr. Tulia Ackson.



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form