RAIS MAGUFULI AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA KITUO CHA MABASI HARAKA

"Mkurugenzi wa Jiji wewe ndiyo ulisaini mkataba huu, nataka kabla ya mwezi wa 11 mradi huu uwe umemalizika, wafanye kazi usiku na mchana umeme upo, maji yapo, fedha zipo hakuna sababu ya kusingizia Corona mbona hawajavaa barakoa hapa" Rais 


“Haiwezekani Watu wasingizie visingizio vya Corona, kesho mtasingizia mvua, keshokutwa jua, Waziri huyu Mkandarasi aanze kukatwa pesa za kuchelewa kukabidhi mradi (Stand Mbezi Luis), nimeumbwa kusema ukweli na nazungumza mbele ya Askofu Mstaafu Chakwera” Rais

"Ninajua Mkuu wa mkoa ( Dar es Salaam) wewe ni mgeni hapa lakini badilika uwe mkali usiwe sheikh au Askofu, ni lazima watu watimize wajibu wao, Niwaeleze huu mradi nitaufuatilia vizuri, halafu mtaona kama hamtatapika kama kuna hela zozote mlizoziweka, nimeangalia vizuri site Bilioni 71 ni nyingi, niseme wazi fedha nilizoidhinisha mimi ilikuwa ni Bilioni 51, leo naambiwa ni Bilioni 71"



Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form