WAARABU WAJIPANGA KUPINDUA UFALME

Saudia: Wanaufalme wagombea madaraka, zaidi ya wanafamilia 20 wakamatwa kwa tuhuma za kutaka kumpindua mrithi wa ufalme



    Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya “Middle East Eye”, mara baada ya kukamatwa kwa Ahmed bin Abdulaziz (Prince Ahmed), kaka wa mfalme wa Saudia, mfalme Salman bin Abdulaziz, wanafamilia wengine 20 zaidi wa familia ya kifalme wametiwa nguvuni kwa tuhuma za kupanga kumpindua mwanamfalme mrithi Muhammed bin Salman.

    Miongoni mwa waliotiwa nguvuni ni pamoja na mtoto wa mwanamfalme Ahmed, mwanamfalme Nayef bin Abdulaziz, mwanamfalme mrithi wa zamani Muhammed bin Nayef na ndugu yake wa kambo Nawaf.

    Katika taarifa hiyo inasema wanafamilia hao wa familia ya kifalme wametiwa nguvuni kwa tuhuma za kupanga njama kwa kushirikiana na vikosi vya kigeni ikiwemo Marekani ili kumpindua mwanamfalme mrithi Muhammed.

    Inasemekana kwamba amri hiyo ya kuwakamata wanafamilia hao ina saini ya mfalme Salmani.

    ==============

    Previous Post Next Post

    Disqus Shortname

    sigma2

    Contact Form