Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi ametoa saa 12 kwa maafisa wa wizara hiyo kurekebisha eneo la benchi la wachezaji wa akiba kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kubaini paa lake limetoboka. Uwanja huo utatumiwa kwa mchezo kati ya Yanga na Simba Machi 8.