Serikali ya Mapinduzi ya #Zanzibar imesitisha kwa muda safari zote za ndege toka Italia kwenda visiwani humo mpaka itakapotoa maelekezo mengine. Hatua hiyo inalenga kupambana na kuenea kwa Coronavirus, ambapo siku za karibuni Italia imeonekana kuwa na ongezeko la maambukizi.