Jeshi la Magereza nchini limesema Kauli zilizotolewa na Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walipotoka gerezani sio za kweli limesema mambo wanayodai kufanyiwa ni utaratibu wa kawaida kwa wafungwa na mahabusu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza Mrakibu Mwandamizi, Amina Kavilondo ambapo amezitaja Kauli hizo kuwa ni pamoja na mateso ndani ya gereza ambapo wafungwa wanaishi kama wanyama na kutokuwa na haki na madai ya kupimwa ukimwi hadharani.
“Taratibu zilizofanywa dhidi yao ni za kawaida na hazijafanywa kwa kuwa wao ni Viongozi wa Chadema ila vimefanywa kwa mujibu wa taratibu za Magereza na vinafanywa kwa kila mfungwa sio kwao pekee” amesema Mrakibu Mwandamizi Amina.
Akizungumzia kuhusu suala la afya na ukaguzi, amesema kuwa jukumu la Magereza ni kuhakikisha Usalama wa Mfungwa na wafungwa na afya wa Mfungwa husika na wafungwa wote na endapo atakutwa na tatizo atakuwa chini ya uangaluzi zaidi kuliko wengine.
“Hao ni viongozi ambao ni wabunge kutumia nafasi yao wanapopita katika Magereza hizo kufanya ukaguzi watumie nafasi hiyo kuzungumzia changamoto hizo ambapo zitapata uzito na kupatiwa ufumbuzi zaidi kuliko kusubiri mpaka wawe wafungwa ndio watoe Kauli hizo” amesema.
Pia amezungumzia kuhusu ukaguzi maalum unaofanywa kabla ya kuingia gerezani kwa kutumia mashine za ukaguzi, mfungwa kupewa shughuli mbalimbali kama kufanya usafi na nyingine, kupigwa kwa virungu kwa mahabusu na tarehe ya Mahabusu kupelekwa mahakamani huku wakidai kuwa mkuu wa Jeshi kukiri kuwa hatoshi kwenye nafasi hiyo.
Amelitolea ufafanuzi ambapo amesema, Kauli hizo haziko sahihi na zinalenga kupotosha utendaji kazi wa Jeshi hilo la Magereza nchini.

Tags
BREAKING NEWS