BEI YA MAFUTA YASHUKA KWA ASILIMIA 30%

Bei ya mafuta imeshuka kwa asilimia 30, kiwango hicho ni kikubwa tangu mwaka 1991 wakati wa Vita vya Ghuba, baada ya Saudi Arabia kuamua kushusha bei.

Hatua hiyo inaonekana kama kujibu hatua ya Urusi kukataa kupunguza uuzaji wa petroli.

Wakati wa mkutano nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi duniani, OPEC, wiki iliyopita, Urusi ilisema haitoungana na wanachama wa OPEC katika juhudi za kuleta utulivu wa soko kwa kupunguza uuzaji wa mafuta.

Mkutano wa OPEC ambao umeijumuisha Urusi, ulipaswa kukubaliana kupunguza uuzaji wa mafuta wa mapipa milioni 1.5 kwa siku, ingawa Urusi ilikataa pendekezo hilo ambalo baadhi wamelielezea kama vita ya kibiashara.

Mpango wa sasa wa uuzaji mafuta kati ya OPEC na Urusi unamalizika mwezi Machi. Saudi Arabia inapanga kupunguza bei yake rasmi ya kuuza mafuta mwezi Aprili kutoka Dola 6 hadi Dola 8.
Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form