Mpiga gitaa wa Bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Mabera aliyeitumikia bendi hiyo kwa miaka 47 mfululizo amefariki baada ya kuugua kwa muda. Mabera Said mtoto wa marehemu amesema mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri Goba, Dar es Salaam.
Tags
BREAKING NEWS