Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JOHN MAGUFULI, ametuma salamu za rambirambi pamoja pesa taslimu Sh. Milioni 5 kwa familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, UVCCM Mkoa wa Iringa Ndg. Emmanuel Mlelwa aliyeuawa.
Pia kupitia kwa katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Dkt.Frank Hawasi, ameagiza vyombo vya Dola mkoani Njombe kuwabaini na kuwachukulia hatua wote waliohusika na mauaji ya Mwenyekiti wa uvccm_vyuoni Ndg. Emmanuel Mlelwa.
Tags
UCHAGUZI