Kulingana na habari katika gazeti la "Washington
Post", Msemaji wa White House Judd Deere amesema kuwa Marekani
haitashiriki katika Mpango wa Chanjo dhidi ya Covid-19 (Covax), ambao
unaratibiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Akisisitiza kuwa Marekani itafanya suala la chanjo peke yake, Deere, amesema
"Marekani itaendelea kushirikiana na washirika wake wa kimataifa
kuvishinda virusi, lakini haitajishirikisha na mashirika ya kimataifa chini ya
ushawishi wa Shirika la Afya Duniani na Uchina."
Utawala wa Donald Trump umetangaza mnamo Mei 29 kwamba umemaliza uhusiano wake
na WHO kwa madai kwamba "Shirika hilo lilifanya maamuzi yaliyoathiriwa na
China katika kupambana kwake na janga hilo".
Mikutano inafanywa na zaidi ya nchi 170 zilizo chini ya mpango wa Covax, ambao
unakusudia kuharakisha juhudi za kutengeneza chanjo ulimwenguni, kuwezesha nchi
zote kufaidika na chanjo na kuwafanya watu walio katika hatari kubwa wanufaike
na chanjo wakiwa wa kwanza.
Mashirika mengi na nchi nyingi zikiwemo nchi washirika wa Marekani kama
Ujerumani na Japan, wameunga mkono mpango huo.
Tags
BREAKING NEWS